Bukobawadau

WATU 6 WAMEUAWA KUFUATIA SHAMBULIZI LA CHUO KIKUU NCHINI KENYA

Mpaka sasa Watu 6 wamedaiwa kuuawa kufuatia shambulizi la chuo kikuu nchini Kenya huku wanne wakijeruhiwa

 Wapiganaji waliofunika nyuso zao wameshambulia eneo la chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa taifa hilo na Somalia.Milio mikali ya risasi pamoja na milipuko imesikika katika chuo kikuu cha Garissa mjini humo.
Maafisa wa usalama wa Kenya wamethibitisha kuwa watu wawili wamefariki huku wanne wakijeruhiwa.
Wakaazi wa eneo hilo wametakiwa kukaa mbali na eneo la chuo hicho.
Haijulikani ni nani aliyehusika na shambulizi hilo ,lakini kundi la wapiganaji wa Somalia Al shabaab limetekeleza misururu ya mashambulizi mjini Garissa pamoja na maeneo mengine ya Kenya tangu mwaka 2011 wakati wanajeshi wa kenya walipopelekwa Somalia.
 Hizi ni picha za matukio ya shambulizi la chuo kikuu cha mji wa Garrissa nchni Kenya ambapo takriban watu 6 wamedaiwa kuuawa kufikia sasa.
 Chanzo:BBC
Next Post Previous Post
Bukobawadau