Bukobawadau

KUHUSU WAKIMBIZI WILAYANI NGARA

KAMATI ya Ulinzi na Usalama mkoani Kagera leo imefanya ukaguzi wa mpaka wake wilayani Ngara na nchi jirani ya Burundi ili kujiridhisha na taarifa za kuingia kwa wakimbizi kutoka nchini humo wanaodaiwa kukimbia maandamano ya kisiasa
Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw John Mongella ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo mkoani humo amesema  wakimbizi walioingia nchini kupitia wilayani Ngara ni raia tisa wa Burundi walioko kijiji cha Kasange mpakani na nchi jirani ya Burundi
Mongela amesema kuwa serikali ya Tanzania kupitia waziri wa mbambo ya ndani ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza kuepo kwa wakimbizi kutoka  nchini Burundi na kuanza  kuwapokea kisha kuwapatia hifadhi kwa ajili ya usalama wao
Amesema  walikokutwa wakimbizi hao tisa wako mpakani na nchi yao ya Burundi lakini wananchi wenzao wa nchi hiyo bado wanaendele na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali jambo ambalo halijatoa fursa kuwapokea mkoani Kagera.

“Sisi tunawaombea wenzetu wa Burundi kuishi kwa amani na endapo wataingia tutawapokea kwa kuwa ni utamaduni wetu watanzania kusaidia walio namatatizo ya kisiasa na changamoto nyingine za kimataifa”Alisema Mongela
Wajumbe wa kamati hiyo  ya ulinzi na Usalama wamelikagua eneo la Lumasi wilayani Ngara  kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kuwapokea wakimbizi ambapo liliwahi kutumika wakati wa wakimbizi wa Burundi kati ya mwaka 1995
 Katika kundi pichani ni sehemu ya Wakimbizi 9 kutoka Burundi walioko kijiji cha Kasange mpakani na nchi jirani ya Burundi.
 Katika hatua nyingine Mongela ameagiza Halmashauri ya wilaya ya Ngara kuacha mara moja kuuza maeneo na rasilimali mbalimbali katika halmashauri hiyo ambazo zinaweza kusaidia wananchi panapotokea majanga ya kijamii
Amesema  rasilimali hizo ni msaada wa baadaye panapotokea matatizo kama majanga ya kuhitaji kupatikana miundombinu na kwamba eneo la Lumasi iliyokuwa kambi ya wakimbizi 1995 hadi 2000 yameuzwa na kugawiwa wananchi
Wakimbizi tisa waliokuwa mpakani mwa kijiji cha Kasange wilayani Ngara na   nchi jirani na Burundi wamesema waliingia Tanzania siku tatu zilizopita na kupewa hifadhi katika kijiji hicho wakitokea mpakani na nchi jirani ya Rwanda
Wamesema wanakimbia nchi yao baada ya kuhojiwa usiku nina kuorodheshwa majina kulazimishwa kutamka kuwa wafuasi wa chama cha CNDD FDD na baada ya muda wanapoamka hukuta majirani zao wameondoka hivyo kujawa na woga
Juzi mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu aliliambia gazeti hili kuwa wakimbizi 85 walioingia wilayani humo wakitokea nchini Rwanda raia wa Burundi wamerudishwa makwao kupitia mpaka wa Kobero nchini humo
 Mkuu  wa idara ya uhamiaji mkoani Kagera  George Kombe amesema idara hiyo inapokea na kuwarudisha  wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyume na taratibu mbapo hadi  Aprili 30  mwaka huu wamerudishwa makwao wahamiaji 175
Amewahimiza wananchi na viongozi wa vijiji wilayani Ngara kushirikiana na vyombo vya dola kuwabaini wahamiaji haramu na kutoa taarifa sahihi endapo watakuwepo wakimbizi kwa ajili ya kupatiwa usalama katika maeneo husika
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera akikagua maeneo yaliopo mpakani Wilayani Ngara.

NGARA:Na Shaaban Ndyamukama

Next Post Previous Post
Bukobawadau