Bukobawadau

VIDEO/PICHA MKUTANO WA DR. SLAA WILAYANI MULEBA LEO JUMATATU MAY 25,2015


Matukio ya picha katika Mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa uliofanyika leo Muleba katika uwanja wa Red Cross.
Katibu Mkuu Dr. Slaa alianza ziara ya siku 3 mkoani hapa toka siku ya jumamosi alipokuwa na Mkutano Mjini Bukoba maeneo ya Hamugembe kisha siku ya jana Jumapili alikuwa Karagwe na leo Jumatatu Wilayani Muleba ikiwa ni sehemu ya majukumu Kichama
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa akisahini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Red Cross Muleba kwa ajili ya mkutano wa hadhara, pichani kulia ni Katibu wa Baraza la Wazee (Chadema)Bwana Rodrick Lutembeka


 Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa Dr.Slaa uliofanyika viwanja vya vya Red Cross Wilayani Muleba leo May 25,2015.

 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa akihutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano huo
Dk. Slaa pamoja na mambo mengine amefafanua umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura licha ya mizengwe inayoendelea kwenye zoezi hilo. Amesema bila kujiandikisha, kuiondoa CCM madarakani ni ndoto.

Dr. Slaa amefafanua ushiriki wa mbunge Tibaijuka katika wizi wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Tegeta escrow. Alisema kile anachoenda nacho akijitetea kuwa amesafishwa ni uongo mtupu na anasikitishwa na msomi na mtu maarufu kama yeye kuwa mwongo. Amesema anachotembea nacho kama dodoki la kujisafisha eti yeye ni msafi, ambacho kimeandikwa kwa lugha ya kiingereza, anachowasomea wananchi kwenye mikutano kimetengenezwa na bodi ya ukaguzi ya shule zake na si taasisi maalum ya ukaguzi. Amesema afafanue kwa uwazi milioni kumi kununua mboga, hiyo mboga ni ya aina gani????!!!

Aidha dk.Slaa ametoa nafasi ya wananchi kuuliza maswali ambapo mwandishi wa habari hizi amemuuliza dk. Slaa akisema, ''mheshimiwa Katibu mkuu, hivi punde umetuonesha watia nia udiwani na ubunge, ni wengi kweli kweli na hiyo ni ishara tosha ya ukuaji wa demokrasia. Je, hawa waheshimiwa wamekuhakikishia kiasi gani kubaki wamoja endapo mmoja wapo atapitishwa? Je, wamekuhakikishia vipi kuwa watamuunga mkono atakayepitishwa kugombea?"
Mheshimiwa dk. Slaa katika kujibu swali hilo aliwataka watia nia wenyewe waudhibitishie umma wa wananchi kama watabaki wamoja au watagawanyika. Kwa pamoja wamejibu, ''Tutamuunga mkono atakayepitishwa"
 Mtarajiwa jimbo la Muleba Kusini  Bwana Rodrick Lutembeka katika ubora wake wakati anaongea na Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Sehemu ya Wananchi katika mkutano huo.


Mkutano ukiendelea pichani anaonekana Ndugu Danstan Paul akichukua kumbukumbu.
 Hassan Milanga Diwani wa Kata ya Muleba Mjini (CUF)




 Mtia nia nafasi ya Ubunge jimbo la Muleba kusini
 Watia nia wa nafasi mbalimbali kupitia UKAWA katika picha ya pamoja
Mmoja wa watia nia akijitambulisha.
PITIA SEHEMU YA VIDEO HAPA CHINI
Next Post Previous Post
Bukobawadau