Bukobawadau

NGARA:MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI

Wauguzi wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kutumia kauli zenye kuwafariji wagonjwa  wakiwa kwenye vituo vya kutolea huduma hatimaye waweze kuaminiwa na jamii na kuwapa matumaini ya kuishi wagonjwa wao
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara Dr  Nelson Rufano ametoa wito huo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi yaliyofanyika kwa kumuenzi Muuguzi mkuu Florence Naitingaly raia wa nchini Italia
Dr Rufano amesema kuwa wauguzi  ndio wanaokaa na wagonjwa muda mrefu na kubaini changamoto zinazowakabili hivyo wakitumia lugha ya upole inaweza kuwatia matumaini wagonjwa na waangalizi wao
Aidha Mwakilishi wa Muuguzi mkuu wa wilayani Ngara Bi Doroth Ntakamulenga amewahimiza wauguzi hao tawi la Nyamiaga kufanya kazi  bila ya kuomba rushwa kutoka kwa wagonjwa na kuweza  kuaminika ndani ya jamii  
Kwa upande wao wauguzi wamesema wanafanya kazi katika mazingira magumu lakini wanahita uvumilivu na subira ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya pamoja kuwakemea wanaojitokeza kudhalilisha taaluma yao
Maadhimisho hayo yaliambatana na Burudani ya muziki kwa wauguzi hao huku baadhi yao wakipatiwa zawadi ya utendaji kazi bora ambapo Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw Patrick Ogo amewataka wauguzi  kujituma na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea bali wajiendeleze kitaaluma
 Maadhimishoya siku ya wauguzi hufanyika kwa kujumuisha wauguzi wa zahanati .vituo vya Afya na Hospitali za serikali na taasisis binafsi lakin kwa mwaka huu wilayani Ngara yameadhimishwa kwa kila taasisi kutokana na ukata wa kifedha na wahusika zaidi kuhudhuria maadhimisho hayo kwa ngazi ya Kitaifa.
 Katika picha matukio ya Burudani yakiendelea.
Next Post Previous Post
Bukobawadau