Bukobawadau

MAELFU WASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA BUKOBA JUNE 3,2015

Maelfu ya watu wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza wa ziwa Magharibu na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Balozi wa Tanzania katika nchi za Jamhuri ya watu wa China, Jamhuri ya watu wa KOREA na jamhuri ya Zaire Katika Miaka ya 1973-1975 Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa aliyefariki Mei 25,2015 huko nchini Marekani na Mazishi yake kufanyika June 3,2015 Nyumbani kwake Kijijini Kitendaguro Bukoba.
Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa aliyewahi kuwa Mbunge wa Wilaya ya Bukoba Mjini kwa kipindi cha miaka 20 na mwenyekiti wa kuchaguliwa wa Halmashauri/Manispaa Bukoba toka mwaka 1975-1985 na MEYA wa Manispaa Bukoba mpaka mwaka 2010.
Pichani waliosimama ni sehemu ya watoto wa Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa, Marehemu alibahatika kupata jumla yawatoto 12 wakiume 6 na wakike 6, kati ya hao  mmoja ameishatangulia mbele ya haki.
Hivyo Marehemu Mzee Luangisa ameacha Mjane (pichani kushoto) watoto 11 pamoja na wajukuu 16.
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa
 Machozi na vilio vikitawalawakati Jeneza lenye Mwili likiingizwa Kaburini.
 Kampuni maalum ya Mazishi kutoka nchini Uganda 'Uganda Funeral Services' ndiyo inayotoa huduma katika shughuli hii
 Safari ya mwisho ya maisha ya Marehemu mzee Samuel Ntambala Luangisa (83 ) aliyewahi kuwa mfanyakazi katika Wizara ya  mambo ya nchi za nje na ofisi ya Waziri Mkuu , Mwaka 1975 aliteuliwa kuwa Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la  Kujenga Taifa.
Sehemu ya Wanachama 'Pamoja Group' katika huzuni mkubwa.
 Tunapata neno la familia ya Marehemu kutoka kwa mwanae Mr Mao Samuel Luangisa
 Askofu Mkuu Mstaafu na kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ... Tanzania (KKKT), Dk. Samson Mshemba.
 Bishop Elisa Buberwa
 Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa
 Viongozi wa Dini walioshiriki Maziko hayo nyumbani Kijijini Kitendaguro Bukoba
 Wanahabari wa vyombo mbalimbali
 Muendelezo wa matukio katika mazishi ya Marehemu Mzee Samuel Luangisa (1932-2015)
 Sehemu ya wafiwa pichani
 Sehemu ya Viongozi wetu wa Dini mbalimbali
Bi Jeanifer Murungi Kichwabuta akitoa neno kwa niaba ya Watoto wa Marehemu waishio Bukoba.
Salaam za rambirambi kutoka Mji wa Nykobing Mors zinatolewa na  Mzee Rutabingwa.
Mwalimu Bilkhes akiongea kwa niaba ya Mzee Abbakar Galiatano
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mjini
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.John Mogella akitoa Salaam za rambirambi kwa niaba ya Rais Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
 Salaam za rambirambi kutoka kwa Viongozi wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini
 Mwakilishi wa Uongozi wa Kamati ya Ulinzi Mkoa.
 Uncle Salum pichani na Uncle Majid Kichwabuta.
 Sehemu ya umati wa waombolezaji.
Matukio mengine zaidi ya picha yanapatikana katika ukurasa wetu wa facebook.
 Mpambambana ji Samuel Lugemalila pichani Kushoto na Mr Al Amin Idrisa (Kada)
 Huzuni,Simanzi na Majonzi Vikitawala 
 Mama Mody pichani mmoja wa waombolezaji
 Hakika ni moja kati ya Shughuli ya maziko tunapata kushuhudia kwa wingi wa watu na mpangilio
 Mc Rutakwa Muongozaji wa Shughuli nzima
 Sehemu ya waombolezaji walijitokeza kushiriki mazishi ya Mpendwa wao Marehemu Mzee Luangisa.
 Mr  & Mrs Christopher Chichi
 Mama Ashura pichani mmoja wa wanakati wa shughuli ya maziko haya.
 Sehemu ya waombolezaji pichani anaonekana Mama Peter Mulima
Sehemu ya Wanafamilia pichani
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki akiweka maua kaburini
  Mbunge wa muleba kusini Prof Anna Tibaijuka akiweka maua katika Kaburi la Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa.
 Mzee Pius Ngeze
Mr. Majid Kichwabuta akiweka maua katika kaburi.
Mama Hassan ( Hawa) na Mama Farida.


Mr Mao Samuel Luangisa na Dada yake Eunice Samuel Luangisa
Wanakwaya wa CHUO CHA UALIMU ERA wakiimba nyimbo za maombolezo
 Watoto wa Marehemu wakiweka maua katika Kaburi.
 Mr George Lwakatare na Mr. Ben Man Mulokozi.
 'Mwanadamu tukumbuke sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi'... Mchungaji akiweka Udongo kaburini.
 Mjane wa Marehemu akiweka Udongo.
 Mama Vick muakilishi wa familia ya Lugakingira
 Mchungaji akiwa tayari kuwekamsalaba kwenye kaburi la marehemu Mzee Samuel Luangisa
 Mr. Bigambo Diwani wa kata ya Bakoba
 Mh. Mkuu wa Mkoa na Mke wake pichani

Ni Simanzi kubwa kwa wanafamilia , tumuombe Mungu aipokee roho ya Marehemu mzee Luangisa
 Mr & Mrs Badru Kichwabuta
 Mama Lugusha pichani kushoto akishiriki Ibada ya Mazishi ya aliyewahi kuwa Mkurugenzi bodi mbalimbali kama Balimi, Shirika la Taifa la Mafuta ya Petroli na Shirika la Utalii na Uvuvi.
 Taswira mbalimbali kupitia Bukobawadau Blog June 3,2015
Pichani kushoto ni Mr Jack (Jack almasi)
 Mr Kwame na Peter watoto wa Marehemu Mzee Samuel Luangisa wakiweka shada la maua.
 Ms Rose Samuel Ntambala Luangisa akiweka shada la maua kwa niaba ya watoto wa Kike.
 Dada Mecy na Da' Farida kwa pamoja wakiweka shada la maua.
 Mr.Ben Mulokozi akiweka shada la maua kwa niaba ya marafiki wa familia
 Ndugu wa Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa wakiweka Shada la Maua
 Kwa niaba ya Wanapamoja Group Mama Mwainunu na Mr.Jamal Kalumuna wanaweka shada la maua
Mr Archard kwa niaba ya  Rotary Club Bukoba
Lujwangana family.
 Baba Askofu Methodius Kilaini akiweka shada la Maua
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta akiweka shada la maua.
 Mrs Chichi akiweka shada la maua
 Mr. Salum Organizer akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Marehemu kipenzi cha wengi Mzee Samuel Luangisa
 Mr. Mrs Badru Kichwabuta
 Mzee Rutabingwa akiweka shada la maua kwa niaba ya  SAGUTI family
Mr & Mrs Majid Kichwabuta wakiweka shada la maua.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye akiweka Shada la Maua,
Mc no 2. muongozaji wa Shughuli ya maziko haya.
 Zoezi la kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la Marehemu mpendwa Wetu mzee Samuel Luangisa
 Taswira mbalimbali kama inavyojionyesha pichani
 Haji Adam, Mr Super Mkude, Mh. Kilaja  na Ndugu Felix Mulokozi pichani
 Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea
Kwa niaba ya Wajukuu shada ya maua anaweka Ms Shamila Majid Kichwabuta
 Mrs Jalia Mayanja katika picha na Mdogo wake Mrs Deo Lutinwa ( Kamama).
 Wakati Mr William malecela le mutuz akiweka shada la maua
 Kuelekea mwisho kabisa ndivyo wanavyo onekana sehemu ya waombolezaji
 Salaam za rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa KCU 1990 LTD
 Pichani anaonekana Ms Rose Samuel Luangisa.
 Ikumbukwe Marehemu Mzee Luangisa amekuwa kadawa Chama cha mapinduzi mwaminifu na Muasisi katika kipindi cha maisha yake yote
 Kama wanavyo onekana kidotcom zaidi.
Mzee Masabala akitoa neno.
 Mzee Baruti rafiki wa karibu wa Marehemu Mzee Samuel Luangisa
 Kwa namna ya pekee hazina ya Wazee tuliobaki nao Mjini hapa Mzee Abdulziad Kashinde anatoa neno na historia fupi alivyo mfahamu Marehemu Mzee Samuel Luangisa 
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera pichani kushoto John Mogella na Mh. Mbunge Balozi Khamis Kagasheki wakimsikiliza kwa umakini Mzee Abdulziad Kashinde.
 Dada Passycazia Barongo akitoa neno
 Dada Farida Kassim na Ms Shamira Majid Kichwabuta pichani
Mhashamu Methodius Kilaini akitoa Salaam za rambirambi na histofia fupi ya Marehemu Mzee Luangisa
 Mr. Kwame akitoa neno laShukrani  kwa niaba ya watoto wa Marehemu Mzee Luangisa
Mr Christopher Chichi akitoa neno kwa niaba ya familia ya Nyamwihura.
Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa ndiye aliyekuwa katibu wa TANU wa kwanza wa  Ziwa Magharibu.
Kwaya ya Chuo cha Ualimu ERA.
Mr Sunday mara baada ya kushiriki mazishi ya Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa.
 Katika picha ya kumbukumbu sehemu ya wanafamila
 Wanapamoja katika picha ya kumbukumbu
 Haya yote yaliyoahinishwa kupitia Bukobawadau Blog, Marehemu Mzee Samuel Luangisa aliyafanya kwa sababu ya moyo wake wa uzalendo kwa Taifa lake, Chama chake na watu wote wa Tanzania
Moja ya picha ya kumbukumbu kwa Waombolezaji
 Mzee wa 'Bwishokogoto' Mr Kagunguna pichani.
Haya ndiyo yaliyojiri katika shughuli ya Mazishi ya Marehemu Mzee Samuel Ntambala Luangisa Mwenyekiti mwanzilishi wa Bukoba Sistership Promotion Trust Fund chombo ambacho kinastawisha udugu kati ya Morsoe, Denmark na Manispaa ya Bukoba tangu mwaka 1983 hadi sasa.
*Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe*
 BASI KAMA TUKIISHI AU TUKIFA,TU MALI YA BWANA WARUMI 14:8
 MATUKIO YA PICHA 200 TAYARI YANAPATIKANA KATIKA UKURASA WETU WA FACEBOOK KUPITIA LINK HII BUKOBAWADAU MEDIA

Next Post Previous Post
Bukobawadau