Bukobawadau

SABA WAFARIKI DUNIA AJALI YA GARI RUVUMA

Wanafunzi sita wa sekondari ya Makatekista na mkuu wa sekondari hiyo Padri Hyasinti kawonga wamefariki dunia na wengine ishirini na sita  kujeruhiwa kati ya hao wanne hali zao zikiwa mbaya baada ya gari aina ya Landrover wanten kutumbukia kwenye korongo na kuwaka moto  katika kata ya Kigonsera wilayani Mbinga  mkoani Ruvuma.
ITV imefika eneo la tukio Kigonsera wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma na kushudia kijiji cha Kigonsera kikiwa katika hali ya simanzi ambapo mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kigonsera Dkt Patrick Mhagama amesema wamepokea miili saba na majeruhi ishirini na sita na kwamba miili imeunngua vibaya kiasi cha kushindwa  kutambulika baada ya gari hilo aina ya Landrover wanten kuwaka moto.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema ajali hiyo ilitokea baada ya kufeli breki na derva ambaye alikuwa marehemu Padri Hayasinti Kawonga akakata kona ndipo alipoingia kwenye korongo na ikatokea shoti na gali likawaka moto huku hilo likiwa ni tukio la tatu katika miaka tofauti kuua watu saba ambapo kuna wanajeshi saba walikufa kwa ajali ya gari na kufuatiwa na ajali ya maji ilioyoua watoto saba waliosombwa na maji katika kata ya Kigonsera.
 
Mwenyekiti wa kitongoji cha misheni katika kata ya Kigonsera Bw. John Kafarapia amesema ni pigo kufiwa na padri Kawonga aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari ya Makatekista na mfadhiri wa wananchi mbalimbali.
CREDIT ITV

Next Post Previous Post
Bukobawadau