Bukobawadau

MAELEZO YA BALOZI KAMALA KATIKA MKUTANO WA KURA ZA MAONI UBUNGE JIMBO LA NKENGE

Mgombea ubunge Jimbo la Nkenge kwa tiketi ya CCM,Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya, Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiongea na wananchi waliohudhuria mkutano wa wa Wagombea Ubunge mchakato wa kutafuta kura za maoni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi  Katano Kata ya Ishozi -Missenyi siku ya jana.
Katika jitihada za mahamasisha maendeleo Balozi Kamala anasema alifanya mambo yafuatayo alipokuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge:
  • Alianzisha Mkutano wa Wadau wa Maendeleo wa kila mwaka
  • Alianzisha Mkutano wa Wadau wa Maendelea wa Jimbo la Nkenge kwa wadau wa maendeleo wa Jimbo hilo wanaoishi nje ya jimbo.
  • Alianzisha utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara jimboni katika kata zote kabla na baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge.
  • Alichangia  mifuko ya simenti 5000 (elfu tano) yenye thamani ya shilingi za kitanzia Milioni 100 kuhamasisha ujenzi wa Sekondari.
  • Alianzishisha kilimo cha  mpunga wa nchi kavu kama zao la nyongeza la biashara.
  • Alihamasisha kuanzishwa kwa vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS)
  • Alitafuta fedha za kitanzani milioni 110 zilizowezesha kujenga ofisi za SACCOS katika Kata zote za Jimbo la Nkenge.
  • Alichapisha kitabu kitabu kiitwacho ''The Voice of the Poor and Poverty Eradication Strategies in Tanzania'' chenye Internation Standard Book No. 90 20 34 414 kuhakikisha hoja za wakulima wa kahawa zinafika kwa watu wengi Duniani.
  • Alimwezesha mtaalamu wa kutoa Elimu ya kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS).
  • Alisambaza  vitabu kwenye sekondari zote Jimboni Nkenge vyenye thamani ya fedha za kitanzania shilingi milioni 100. 
MSIKILIZE BALOZI KAMALA KATIKA (AUDIO) AKIONGEA NA WAKAZI WA ISHOZI Muendelezo wa matukio yaliyojiri katika Mkutano huo.
 Mdau wa maendeleo ya Jimbo la Nkenge Ndugu Samuel Lugemalila (kushoto) akibadilishana mawazo na mwananchi aliyehudhuria mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi  Katano Kata ya Ishozi Wilayani Missenyi
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia mkutano huo,pichani kushoto ni Mzee Yassin.
 Pichani ni jumla ya wagombea ubunge sita CCM Jimbo la Nkenge.
(Ishozi-Nkenge) pichani ni wagombea Udiwani ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),kutoka kushoto ni Mzee Alex Tibita na Ndugu William Osward.
 Ndugu P. Matunda akifanya mrejesho kwa njia ya simu kuhusu yaliyojiri katika mkutano huo.
 Wadau wakibadilishana mawazo.
Hakika siasa za Jimbo la Nkenge zinagusa hisia za watu wengi katika makundi mbalimbali
 Umati wa watu waliohudhuria mkutano wa Wagombea Ubunge mchakato wa kutafuta kura za maoni uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi  Katano  Ishozi-Missenyi.
 Ndugu Shitobelo Emmanuel, katika wa Vijana CCM Missenyi akitolea jambo ufafanuzi.
 TUJIKUMBUSHE WAKATI BALOZI DK DIODORUS KAMALA AKIONGEA NA WANAHABARI WIKI MBILI ZILIZOPITA BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA MWISHO:BUKOBAWADAU MEDIA tunafurahia kuwa na uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241 SEHEMU YA VIDEO
Next Post Previous Post
Bukobawadau