Bukobawadau

VIP KUSHIRIKIANA NA COSAD CLINIC NA MADAKTARI WALIOPO BUKOBA KUBORESHA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA VIPIMO

Mshauri wa kimataifa  wa kujitegemea wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd Fr. James Rutakwabyera pichani katika akizungumza katika kikao cha washauri wa ndani wa kampuni wa VIP wanaoishi Mjini Bukoba.
 Adv Steven Byabato ambaye ni kati ya washauri wa ndani wa kampuniVIP Engineering and Marketing Limited,akitolea jambo ufafanuzi.
1.      VIP ikiongozwa na taarifa za kitafiti kuhusu hali ya ugonjwa wa Kansa katika Tanzania na hususani ukweli kwamba maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria yana unyemelezi mkubwa wa magonjwa ya kansa tumejihusisha kufuatilia ukweli huo na kubaini kwamba pia lipo tatizo kubwa la magonjwa ya saratani ndani ya Mkoa wa Kagera.

2.      Wakati VIP ikiendelea na mchakato wa kupata ardhi katika eneo la Kitongo-Makongo ndani ya Manispaa ya Bukoba, kwa ujenzi wa hospitali kubwa ya kimataifa kwa ajili ya kuchunguza na kutibu maradhiya saratani. tumegundua kwamba lipo tatizo la kitaalam la kuchunguza na kutambua magonjwa ya aina mbali mbali.  Tatizo hili linaonekana zidi kuwa kwenye maeneo makuu mawili:

i).  Vifaa tiba vya kupima magonjwa mbali mbali zikiwemo mashine na kemikali (reagents).

ii). Uhaba wa Madaktari na wataalam wa mahabara kuwahudumia wagonjwa.

3.      VIP inatambua na kuthamini kwamba ni watu walio na afya njema wanaoweza kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za ujenzi wa Taifa.  Pamoja na ukweli huo, bado yapo maradhi ambayo hayahepukiki na mengine yanatokana na jinsi na namna ya maisha yetu ya kila siku (life style). Lakini pia ni ukweli kwamba mtu akipata maradhi kwa sababu yeyote ile, basi ili aweze kupatiwa tiba sahihi anapaswa awe amefanyiwa uchunguzi ulio sahihi ili kugundua tatizo lake.

4.      Ni dhahiri kwamba baadhi ya magonjwa hutokea yakawa sugu na hata kupelekea kwenye magonjwa hatari ya kansa pale yanapokosekana kutambuliwa na kupatiwa tiba sahihi kwa wakati ulio sahihi.  Kwa hiyo ili kukabiliana na tatizo hilo, VIP inapanga kuanzisha ushirikiano na COSAD Clinic inayoendesha Zahanati ya kisasa yenye mashine za kisasa za kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa magonjwa mbali mbali, iliyopo hapa Kashai ndani ya Manispaa ya Bukoba.

5.      Aidha ushirikiano huo utaongezwa nguvu na washirika wengine muhimu ambao ni madaktari sita ambao wanafanya kazi kwenye hospitali na taasisi mbali mbali hapa Mkoani Kagera. Madaktari hao wataombwa kushirikiana na Madaktari wa COSAD, Inc. kutoa huduma kwenye Kliniki ya COSAD kwa kadiri watakavyojipangia.  Ratiba yao itatangazwa kwa wananchi wote kwa  njia mbali mbali za mawasiliano.  Tunakusudia huduma hii ianze ifikiapo tarehe 15/08/2015.

6.      Ili kuwezesha huduma za vipimo mbali mbali kuweza kuanza kufanyika kwenye maabara ya COSAD, Inc. VIP Engineering and Marketing Ltd., kwa kuanzia imetoa msaada wa (reagents) zenye thamani ya TZS. ………….. kwa COSAD, Inc. kliniki

7.      Kwa wakati muafaka VIP itashirikiana na viongozi wa ngazi zote katika wa Mkoa na wadau wengine kwenye mpango wa kuhamasisha juu yakupambana na ugonjwa hatari wa sratania ambao kwa sasa unaongoza kwa kuyachukua maisha ya watanzania katika rika zote, watoto, vijana, kina mama, wakina baba na wazee hapa nchinina hata katika nchi jirani.
 Adv AaronKabunga  Mr. Frank Rutemerwa  timu ya washauri wa VIP

8.      Tatizo la kuongezeka kwa vifo vinavyotokana  na saratani limeendelea  kuwa ni uelewa mdogo wa jamii juu ya ugonjwa huo, ambao husababisha wagonjwa wengi kugundulika wakati kansa imekwisha sambaa sana kwenye mwili na hivyo wagonjwa hao kutokuwa na uwezekano wa kupona.
9.Ni imani ya VIP kwamba kushirikiana kwa dhati katika mpango huu, tunaweza kutoa mchango mkubwa kunusuru maishaya watu wengi wakati tukielekea kujenga hospitali kubwa ya kimataifa ya kuchunguza na kutibu magonjwa ya kansa, Rutakwabyera International Cancer Centre and The Intergrated Medical Tourism Eco Village.
 Mr&Mrs Remidius (Dokta Remmy) wakurugenzi wa Smart Hotel kilipofanyika kikao cha VIP.
 Mshauri wa VIP Mwl. Saada Juma pichani katikati  akiteta japo na mwakilishi wa VIP Mr. Rahym Kabyemera
 Fr. James Rutakwabyera katika picha na Adv .Josephat Rweyemamu mshauri wa ndani wa VIP.
VIP inawaomba wananchi wote kuwaunga mkono
Imetolewa Bukoba,  tarehe 4 Agosti, 2015 na;
Fr. James Rutakwabyera
Mshauri wa kimataifa  wa kujitegemea
VIP Engineering and Marketing Ltd
Next Post Previous Post
Bukobawadau