Bukobawadau

LOWASSA KAMA LULU TANGA

Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Mh.Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano mjini Tanga baada ya maelfu ya wakazi waliojitokeza kushindwa kuenea ndani ya uwanja wa Tangamano jijini Tanga.
Kwa mara ya kwanza ndani ya jiji la Tanga shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5,6,7, 8  zililazimika kusimama kwa muda baada ya maelfu ya wakazi wa jiji hilo waliojitokeza katika uwanja wa Tanagmano, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea kwa mkutano huo.

 Licha ya juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo kushindikana jambo lililomlazimu Mh.Edward Lowassa kulazimika kusitisha mkutano huo.
Je? Nini kauli ya Chadema baada ya mkutano huu kuvunjika, John Mrema ni meneja kampeni wa Chadema.

Uamti huo wa wakazi wa jiji la Tanga ulionekana dhahili  ulionekana dhahili kuwashinda maafisa wa taasisi ya mslaba mwekundu redcros mjini Tanga.
Akiwa jiji Tanga katika siku yake ya kwanza ya kampeni alifanya mikutano katika maeneo ya Bumbuli Mombo kabla ya kuhitimisha katika uwanja wa Tanagmano mjini Tanga ambapo aliahidi kuboresha sekya ya afya ndani ya siku miamoja baada ya kuapishwa.
 LOWASSA APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIMBO LA BUMBULI, MKOANI TANGA
Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakimlaki kwa shangwe Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Kisiwani, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo leo Septemba 28, 2015.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Soni katika Jimbo la Bumbuli, wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwani, leo Septemba 28, 2015.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kisiwan, Mji wa Soni katika Jimbo Bumbuli, Mkoani Tanga leo Septemba 28, 2015.


Next Post Previous Post
Bukobawadau