Bukobawadau

MWILI WA MAREHEMU BI ZAITUNI KABYEMELA WASINDIKIZWA KUELEKEA NYUMBANI MARUKU

 Matukio ya picha baada ya mwili wa marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela (Mama Rahym Kabyemela) kutolewa mochwari ya hospitali ya Mkoa upokuwa umehifadhiwa na mara baada ya Mwili kusaliwa katika msikiti wa Jamia Mjini hapa
 Muonekano wa matukio ya picha baadhi ya waombolezaji na wafiwa wakiwa tayari kwa msafara kuelekea Kijijini Maruku,Mwili wa Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela utapumzishwa katika nyumba yake ya milele siku ya kesho/leo Ijumaa Jan 8,2016 Nyumbani Kijijini Maruku saa 8:00 mchana ( baada ya Sala ya Ijumaa )
Baadhi ya waombolezaji wakiwa tayari kuelekea msibani Kijijini Maruku
 Sheikh Haruna Kichwabuta akiendelea kumfariji Mzee A.Kabyemela kufuatia msiba huu wa Mke wake.
Hakika ni simanzi kubwa kwa watu wote msibani hapa
Pichani kutoka kushoto Bi Maua Ramadhan,Lilian Mwise, Opp Kasimbazi wa Makoko,Optaty Henry (katibu wetu maswala ya Kijamii),Ndg Jamal Kalumuna, Ndg Mwinyi (tshirt yenye mistari) na Bi Rukia  pichani mbele
 Matukio mwili wa Marehemu ukitolewa kwenye Gari.
 Jeneza lenye mwili wa Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela likipelekwa ndani
 Ni vilio na huzuni mara baada ya mwili kuwasili nyumbani Kijijini Maruku
Machozi na Vilio vikitawala kwa kuondokewa na mpendwa wao Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela
 Bi Hawa Hassan na Mama Rubby mara baada ya kuwafariji wafiwa
Bwana Optay akitoa mkono wa pole kwa wafiwa
Mmoja wa watoto wa Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela
Bi Sharifa Karwani pichani
 Baadhi ya wanafamilia wakibadilishana mawazo  msibani hapo.
Kushoto ni Yunus Kabyemela, Khamis Chappa na Bw. Lawrence Barongo
Taswira Kijijini Maruku  baadhi ya wadau walioshiriki kuusindikiza mwili wa Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela
 Mrs Optay akiwa amefika kuwafariji wafiwa
Eneo la maegesho
Mama Hawa Hassan na Mama Rubby pichani
Muendelezo wa matukio ya picha

 Pichani kulia anaonekana Bw. Rahym Kabyemela akijadili maswala  na Dada zake .
 Msafara wa Magari kuelekea Kijijini Kanyangeleko Maruku
Msafara kuelekea Maruku.
Ndivyo anavyo onekana Ndg Optaty Henry mara baada ya kuwasiri Kijijini Maruku
Sehemu ya waombolezaji
Kijana Razackakiendelea kupasha habari za kifo cha Bibi yake
Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela wakati wa Uhai wake
Bukobawadau Media tunatoa pole zetu za dhati kwa familia ya Mzee Kabyemela,
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aipokee roho Marehemu Bi Zaituni K. Kabyemela aipumzishe kwa amani !!
"INNALILAHI WA INNA ILAYHI RAJIOON".!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau