Bukobawadau

NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AZINDUA AIRTEL FURSA TUNAKUWEZESHA MSIMU WA PILI JJINI DAR ES SALAAM LEO

 Naibu Waziri  wa Kazi Vijana na Ajira, Athony Mavunde (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (katikati), na Mshauri wa mradi wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, Mhandisi George Mulamula (kulia), wakiwa wameshika bango linaloonesha Airtel Fursa wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa Airtel Fursa Tunakuwezesha uliozinduliwa leo Makao Makuu ya Artel Tanzania, Moroco  jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso, akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi.
 Mshauri wa mradi wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, Mhandisi George Mulamula akizungumza kwa ufupi kuhusu mradi huo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mradi wa Airtel Fursa Tunakuwezesha katika kipindi cha nusu mwaka na awamu ya pili.
 Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
 Mjasiriamali Mohamed Kigumi aliyenufaika na mradi huo akielezea mafanikio aliyonayo na changamoto anazokumbana nazo baada ya kuwezeshwa na Airtel.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Na Dotto Mwaibale

Kampuni ya simu ya mkononiya Airtel leo imezindua msimu wa pili wa mradi wake wa kuwawezesha vijana ujulikanao kama "Airtel FURSA" kwa lengo kuendelea kudhihirisha kutimiza dhamira yake kuendeleza huduma za kijamii nchini Mradi wa "Airtel FURSA" ulizinduliwa Mei 2015, ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA"  umewawezesha vijana zaidi ya 2500 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kupata mafunzo ya biashara na wengine 13 wafanyabiashara chipukizi wanaofanya vizuri zaidi kupokea vifaa vilikvyowasaidi kuboresha biashara zao na kutengeneza fursa zaidi kwa jamii inayowazunguka.
 

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi mkuu wa Airtel  Sunil Colaso, alisisistiza dhamira ya kampuni yake  kuwawezesha vijana na kutambua mchango walio nao katika kuendesha uchumi wa Tanzania
 

" Mradi huu wa "Airtel FURSA"  unadhihirisha dhamira yetu ya kuwawezesha vijana wa kitanzania wenye malengo ya kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao. Msimu wa kwanza wa "Airtel FURSA" umetoa matokeo mazuri sana na  tumefanikiwa  kugusa maisha ya  maelfu ya vijana wengi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini,"
 

"Katika msimu huu wa pili tunawekeza takribani  shilingi  billion moja ili  kuweza kufikia vijana wengi zaidi ambao wako tayari kutumia fursa na vipaji vyao. Tutaendelea kuwapatia mafunzo ya kibiashara, misaada ya vifaa na kuanzisha mfumo wakisasa wa mafunzo kupitia simu zao za mkononi" alisema Colaso
 

Akizindua rasmi mradi wa "Airtel FURSA" Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde aliwapongeza Airtel kwa kuanzisha  na kuwekeza kwenye mradi huu mkubwa na kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ili kuboresha maisha yao. alisema Mh Mavunde
 

"Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali, zikiunganishwa pamoja na fulsa zinazoletwa na miradi kama hii ya"Airtel FURSA" ni wazi vijana wenye malengo Dhahiri ya kujiendeleza wataweza kuboresha maisha yao. Napenda kuwahasa vijana wetu kutumia fursa hii na kufanya kazi kwa bidii:"
 

"Serikali chini ya Wizara yetu na itaendelea kushirikia Airtel na kufanya kazi kwa pamoja huku ikiweka mazingira bora yatakayochochea vijeza ana kupata fursa ili waweze kuchangia katika kuendeleza  uchumi wa nchi" aliongeza Mavunde"

Airtel FURSA"  ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa  ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. 
Unaweza pia kutuma maombi yako kwa kupitia barua pepe ya airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. Or tembelea tovuti yetu ya  www.airtel.com<http://www.airtel.com>  naujaze fomu yako ya maombi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Next Post Previous Post
Bukobawadau