Bukobawadau

NI VIATU VYA DOLA ELFU 12 VYA MSANII JOSE CHAMELEONE

Wewe ukijikakamua zaidi unaweza kutoa pesa ngapi kununua kiatu....?
Haya basi ,mwanamuziki maarufu kutoka Uganda Jose Chameleone amenunua jozi moja ya kiatu kwa kulipa dola elfu 12 na nusu .
Sasa wengine wanadai eti anajionyesha kuwa anazo.
Lakini yeye anasema ameamua kuzawadi miguu yake!
Muimbaji huyo wa wimbo wa ''Wale wale, waliobarikiwa na mungu '' anasema sio majivuno kamwe bali ni njia yake ya kumshukuru mungu kwa kumjalia na kumpa uwezo kama huo.
Wimbo huu wake wa hivi karibuni umetazamwa na watu zaidi ya milioni moja laki tatu katika mtandao wa Youtube kote .

Juzi alipokuwa ziarana nchini Kenya, aliwaacha watu vinywa wazi kwani aliweka mtandaoni picha ya vyatu vyake aina ya Nike Air Mag.
Jozi hio ya viatu vya nike alinunua kwa dola 12,500 za kimarekani.
Hebu fikiria Chameleo ka nunua kiatu kwa jozi moja kwa pesa sawa na milioni moja na laki tatu za Kenya au karibu milioni 26 za Tanzania.
Mwenyewe kasema anajipa raha, ''jifurahishe ungali hai'', Chameleoni anasema.
Amefafanua kuwa anarudishia miguu yake shukran ''kwa kusimama naye'' na kumuwezesha kufika alipoa sasa.
Chameleon anakumbusha kuwa miaka minane iliyopita nusura awe kiwete kutokana na ajali mbaya.
Sasa amepona na pesa ziko ''kwanini nisishukuru miguu yangu ?
Kwa mahasidi wake wanamzomea eti anajionyesha na kufuja pesa.. Chameleon anawapa ushauri kuwa ikiwa hawawezi kutoa dola elfy 12 mia tano kununua kiatu . Basi wachina wanauza viatu bei rahisi sana...wasimuonee sooo wakanunue viatu saize yao mali ya wachina.
Next Post Previous Post
Bukobawadau