Bukobawadau

CCM YATAKA WAKURUGENZI MANISPAA YA ILALA, KINONDONI WAWAJIBISHWE KUCHELEWESHA UCHAGUZI WA MEYA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam kimemuomba Waziri Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene kuwawajibisha Wakurugenzi wa Manispaa ya Ilala na Kinondoni kwa kile walichodai ni kuvuruga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Hayo yalizungumzwa Dar es Salaam jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar e Salaam, Juma Simba 'Gadafi' wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kumekuwa na sintofahamu hadi sasa kuhusiana na uchaguzi huo kutokana na woga wa wakurugenzi hao ambao wameshindwa kujiamini.

" Wakurugenzi hawa ndiyo chanzo cha vurugu katika uchaguzi huu wa meya tumewaomba wakurugenzi hawa watoe tamko na tafsri sahihi ya ushiriki kwa wajumbe wenye sifa ili kuacha kuupotosha umma juu ya uchaguzi huu,"alisema Gadafi.

Gadafi alisema kuwa wakurugenzi hao kwa makusudi na huku wakifahamu wanakiuka sheria waliruhusu baadhi ya maswahiba wao kutoka chama cha upinzani ( Ukawa) ambao walitoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam kuingia kwenye uchaguzi uliovurugika.

Gadafi alisema mwanachama yeyote wa CCM anaruhusiwa kufanya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kupingwa kama taratibu unavyoelekeza.

Alisema hizi kauli zinazotolewa kuwa haiwezekani wajumbe wakatoka nje ya Dar es Salaam na kupiga kula eneo lingine hazina ukweli wowote kwani siku za nyuma ziliwahi kufanyika kwa vyama vingine lakini hakukuwa na kulalamika.

Aidha katika hatua nyingine Simba amesema Meya wa Ukawa walioshinda katika Manispaa za Kinondoni na Ilala wanatakiwa watambue kuwa Halmshauri hizo hazitaendeshwa kwa ilani ya chama chao bali ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa asilimia 60 ya bajeti ya maendeleo inaongozwa na chama. 


Next Post Previous Post
Bukobawadau