Bukobawadau

MAMIA WAUAGA MWILI WA BIBI JOSEPHINE SIMON MSHUBUSI, MAZISHI KUFANYIKA BUKOBA LEO JUMANNE MACHI 22,2016


 Mkurugenzi wa Mabibo Beer, James Lugemarila, (kulia), akziungumza wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Bibi Josephine Simon Mshumbusi kwenye Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Machi 20, 2016. Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Bukoba mkoani Kagera kwa mazishi yatakayofanyika Jumanne Machi 22, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

MWILI wa marehemu bibi Josephine K. Simon Mushumbusi umeagwa leoMachi 20, 2016 kwenye kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania, KKKT, Kijitonyama jijini Dar es Sala na tayari umesafirishwa kwenda kijiji ni kwake, Kashura mkoani Kagera kwa mazishi.
Mrehemu Josephine ambaye alifariki Machi 18, 2016 baada ya kusumbuliwa na malaria kali alizaliwa Mei 2, 1931 kwenye kijiji cha Kashura mkoani Kagera na ameacha watoto kadhaa., .
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilianza majira ya mchana na mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake walifika kwenye ibada hiyo, motto mkubwa wa marehemu, ambaye ni Mfanyakazi wa UTT-PID, Euginia Simon, amesema mazishi ya mama yake yatafanyika Jumanne Machi 22, 2016 kijijini alikozaliwa. Bwana alitoa bwana alitwaa na jina lake lihimidiwe.





Fr. James Lugemalira akimfariji mmoja wa watoto wa Marehemu
Usiku wa Jana Jumatatu Mwili wa Marehemu Bi Josephine uliwasili Nyumbani kwake Mjini Bukoba

BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
Next Post Previous Post
Bukobawadau