Bukobawadau

SASI ZA KIRAI ZATAKIWA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa PEDDEREF, Nuru Saleh, juu ya misingi ya upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya wakati wa sherehe za kutimiza miaka 3 tangu kuanzishwa  kituo hicho, Tarehe 04 Machi, 2016, jijini Dar es Salaam.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb), akikabidhiwa risala na Meneja wa PEDDEREF, wakati wa sherehe za kutimiza miaka 3 tangu kuanzishwa kituo hicho cha upataji nafuu kwa watumiaji wa dawa za kulevya, Tarehe 04 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.
 Mraibu aliyepata nafuu ya utumiaji dawa za kulevya wa Kituo cha Upataji nafuu wa dawa hizo PEDDEREF cha Kigamboni, Kidongoni, jijini Dar esaalam, Bi. Eliza akiwaongoza washiriki wengine kusoma sala ya kukiombea kituo hicho wakati wa sherehe za kutimiza miaka 3 tangu kuanzishwa kwake, Tarehe 04 Machi, 2016.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb),(katikati waliokaa) akiwa na waraibu wa Kituo cha  Upataji nafuu wa matumizi ya dawa za kulevya (waliosimama) wakati wa sherehe za kutimiza miaka 3 tangu kuanzishwa  kituo hicho, Tarehe 04 Machi, 2016, jijini Dar es Salaam (mwenye ushungi) Mkurugenzi wa PEDDEREF, Nuru Saleh. 
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama (Mb) akiagana na   Mkurugenzi wa PEDDEREF, Nuru Saleh, mara baada ya kushiriki sherehe za kutimiza miaka 3 tangu kuanzishwa  kituo hicho cha kutoa huduma ya upataji nafuu kwa waraibu wa dawa za kulevya, Tarehe 04 Machi, 2016, jijini Dar es Salaam.

(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Next Post Previous Post
Bukobawadau