Bukobawadau

ZIARA YA WAZIRI MKUU MH.KASSIM MAJALIWA MISSENYI - KAKUNYU NA KAGERA SUGAR

Ziara ya Mh.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa imeendelea mkoani Kaera,kwa siku ya Jana Waziri Mkuu ametembelea kiwanda cha sukari cha KAGERA SUGAR na kukagua ranchi za Taifa za misenyi (Kakunyu) zilizopo mpakani mwa nchi jirani ya Uganda
 Uzalishaji wa sukari kwenye kiwanda cha Kagera unaongezeka,na Serikali inakwenda kuvipatia nguvu viwanda vya ndani kwa kuondoa kodi zisizokuwa na tija kwenye uzalishaji wa sukari ili viwanda vizalishe sukari ya kutosha.
Kuhusu swala la ranchi za Missenye na Karagwe Waziri mkuu ameaiza za kupitiwa upya na kusema tayari wataalamu wameshaanza kazi hiyo,lengo ni kuhakikisha watanzania wananufaika na ranchi hizi,kwa wawekezaji waliohodhi block kwenye ranchi hizi bila kuziendeleza muda wao umefika wa kuondoka kwenye maeneo hayo kabla hatua zingine za kisheria hazijachukuliwa.
Akiongea na Wananchi waliohudhuria mkutano wa adhara uliofanyika kata Kakunyu jana Jumatatu March14,2016 Mh.Kassim Majaliwa amemwagia sifa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala kwa umahiri wa kuchapa kazi na kwa kutambua kuwa Wananchi wa Missenyi wanauhitaji wa maeneo ya shughuli za kiuchumi.

 Aidha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza waziri wa Kilimo na Mifugo Mwiguli Nchemba kuwanyang’anya vitalu vya ufugaji wawekezaji walivyomilikishwa na kampuni ya ranchi ya taifa kwa ajili ya ufugaji wa kisasa na wa kibiashara ambao wanavitumia kinyume.na malengo ili wagawiwe wananchi.
Waziri mkuu huyo amesema wanaotakiwa kunyang’anywa vitalu walivyomilikishwa ni pamoja na wale walioshindwa kuviendeleza na wanaokodisha maeneo ya vitalu hivyo kwa wageni toka nje nchi wanaoingia hapa nchini na mifugo yao,amesema wageni ndio chanzo cha migogoro kati ya wawekezaji na wananchi, pia amepiga marufuku viongozi wa seriali ngazi za vijiji na kata kutoa vibali kwa wageni toka nje ya nchi kwa kuwa vibali hivyo ndivyo vinawapa uhalali wa kuingiza mifugo yao.
 Kwa upande wake,waziri wa kilimo na mifugo Mwigulu Nchemba ameeleza kuwa serikali kamwe haitamuonea mtu wakati wa zoezi la kuwabaini wanaotumia vitalu kinyume na malengo,amesema zoezi hilo litafanyika kwa umakini mkubwa na halitawasalimisha wanatumia vitalu hivyo kufanya shughuli ambazo niu haramau ambazo ni pamoja na ulimaji wa bangi ukataji miti kwa ajili ya uchomaji wa mkaa.
  Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kakunyu wilayani Missenyi katika ziara ya  Waziri mkuu mkoa wa Kagera Jana Machi 14, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo namna ya Uvunaji wa miwa alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea ghala la kiwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
 Sehemu ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Kagera Sugar
 Blogger wenu katika picha na Balozi Dk. Diodorus Kamala Mbunge wa jimbo la Nkenge ndani ya Kiwanda cha Kagera Sugar katika  ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitolea jambo ufafanuzi mara baada ya kufika katika eneo linalotakiwa kujengwa daraja kati ya Kagera kuelekea Karagwe .
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye ndiye Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Jaskon Msome akimkaribisha Waziri Mkuu kuwahutumia mamia ya watu waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika Kakunyu Missenyi Machi 14, 2016.
 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara
 Baadhi ya wadau katika ziara ya Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa Waziri Mkuu mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
Taswira ya wananchi waliojitokeza eneo la Kakunyu Missenyi  katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
 Mkuu wa Wilaya ya Missenyi,Festo Kiswaga akitolea jambo ufafanuzi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipitia Ramani ya eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda kwenye Ranchi ya Missenyi
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Uganda waishio kwenye mpakani waliovuka mpaka ili kumuona wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma wialyani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
 Ndivyo linavyosomeka moja kati ya mabango
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda kwenye Ranchi ya Missenyi mkoani Kagera Machi 14, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi,Festo Kiswaga.
 Mkazi wa Kakunyu Wilayani Missenyi
Katika hili na lile wanaonekana wadau picha
 Mwisho mara baada ya kuwahutubia Wakazi wa Kakunyu, Ziara ya Waziri Mkuu imeendelea Wilayani Karagwe
Next Post Previous Post
Bukobawadau