Bukobawadau

MTOTO GERTRUDE CLEMENCE ATEMBELEA BUNGE

Mtoto Gertrude Clemence wa shule ya sekondari Mnarani Mwanza Ilemela na wanafunzi wenzake amepokelewa kwa shangwe Bungeni leo baada ya kurejea kutoka New York Marekani Umoja wa .Mataifa alipohutubia baraza kuu la umoja wa mataifa kuhusu mazingira kwa ufadhili wa UNICEF. 
Mbunge wa Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka alishirikiana na Mhe Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mwanza Bi Angelina Mabula ambaye pia ni Naibu  Waziri wa Ardhi kumpokea mtoto huyo.

 Prof Tibaijuka ni Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa mstaafu (retired UN UNDER-SECRETARY-GENERAL). Mama Tiba alisema amefurahishwa sana na kipaji cha mtoto huyo aliyetokea shule za kawaida za kata. Mama Tibaijuka ametoa zawadi ya Shs laki moja kwa watoto hao. 
Kwa taarifa Profesa Tibaijuka ndiye mwanamke wa kwanza Mwafrika kuchaguliwa na Baraza Kuu la umoja wa mataifa kwa kura kuendesha shirika lake. Hiyo ilikuwa   2002 na 2006 na hivyo kuliongoza shirika la makazi duniani UNHABITAT lenye makao yake makuu Nairobi kwa awamu 2 hadi alipoamua kustaafu na kurejea nyumbani 2010.
Next Post Previous Post
Bukobawadau