Bukobawadau

MATUKIO KIBAO YA BUNGENI DODOMA JANA


 Mbunge wa Viti Maalumu, Bupe Mwakang'ata (CCM), Mkoa wa Rukwa, akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) bungeni Dodoma LEO, kwamba serikali ina mkakati gani wa kusimamia fedha asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri kwa ajili ya maendeleo  vijana na wanawake.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akiongoza kikao cha Bunge cha majadiliano ya Bajeti ya Serikali bungeni Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiswali la ni lini ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Nyamagana Mwanza utamalizika. Swali hilo lililulizwa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula
 Mbunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa akiuliza swali bungeni
 Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Makame Mabrawa akijibu maswali ya wabunge.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu maswali ya wabunge
 Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu akiuliza swali bungeni
 Wageni waalikwa wakiwa bungeni dodoma
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mbunge Bwanausi wa Lulindi
 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusufu Hamad Masauni bungeni
 Familia ya Mbunge wa Mafinga Cosato Chumi ikiwa bungeni Dodoma huku ikifuatilia mwenendo wa Bunge
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St Marys Duluti ya Arusha wakiwa bungeni kufuatilia menendo wa Bunge hilo
 Mbunge wa Viti Maalum, Jasmine Tisekwa akichangia mjadala wa serikali
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Mary's Duluti ya Arusha waliotembelea Bunge, Dodoma
 Wabunge wa upinzani wakaitoka bungeni kikao cha jioni kwa kutokuwa na imani na Naibu Spika
 Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mchafu akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali bungeni
 Mbunge wa Igarula, Mussa Ntimizi akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali bungeni
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Karagwe kwenye viwanja vya Bunge
 Andrew Chenge akiwa na Lucy Owenye wakiingia bungeni
 Wabunge wakiingia bungeni

 Wabunge wakitoka bungeni kwa ktokuwa na imani na Naibu Spika
 Mbunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa (CCM) Mkoa wa Mbeaya,akichangia mjadala wa Serikali bungeni
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM), akiuliza swali kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bungeni Dodoma jana, kwamba ni linserikali italisisitiza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),  kuhakikisha Uwanja wa Nyamagana unaotakiwa ujengwe kwa nyasi bandia  unakamilika kwa wakati na kuendeleza malengo yaliyokusudiwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau