Bukobawadau

AJALI YA BASI "OTTA CLASS BUKOBA - DAR"

Watu kadhaa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyotokea wilaya ya Kilosa ikihusisha basi la kampuni ya OTTA CLASSIC
yenye namba DGK T.201 lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea jijini Dar ambalo limegongana na lori la mafuta lililokuwa limepaki pembezoni mwa barabara.
Waliofariki dunia ni pamoja na madereva wawili na wasaidizi wao pamoja na abiria wengine.
Miili ya marehemu imekimbizwa na mingine bado inapelekwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa utambuzi na kwa itifaki ila mahututi wengine wanapatiwa matibabu hapo hospitali ya ST JOSEPH inayomiliikiwa na Kanisa la Roman Catholic.
Rai:Kama una ndugu unahisi au unafahamu alikuwa anasafiri basi fanya mawasiliano naye mapema.
Next Post Previous Post
Bukobawadau