Bukobawadau

JIPE MOYO MWANGA UPO

Ipo tofauti kati ya kupita kwenye magumu na kuishi kwenye magumu. Tunapopita kwenye magumu huwa ni ishu ya kitambo kifupi au msimu fulani. Kuishi kwenye magumu maana yake maisha yako ya muda mrefu yako ndani ya tatizo au matatizo, unaujua mwanzo wa ugumu au tatizo hilo lakini mwisho hauujui. Mara nyingine kwenye ndoa zetu tunapita kwenye magumu, hii ni kawaida na ipo kwa wengi, lakini wapo wanaoishi kwenye matatizo, wanaokaa ndani ya magumu, kila tumaini limekufa, haujawahi kuiona furaha na hata kama uliiona basi ni kwa muda mfupi sana japokuwa ulitazamia sana ndoa hiyo iwe jawabu la furaha kwako. Hata kama umefika hapa, still unaweza kutoka kama wote wawili mkiamua. Jiulize, tatizo langu/letu ni nini? Nini chanzo chake? Nini kimetuingiza kwenye tatizo hili? Je mchango wangu ni upi kwenye tatizo hili? na ni kwa kiasi gani ninaweza kuwa suluhisho la tatizo hili? Hakuna changamoto isiyokuwa na mlango wa kutokea endapo utaamua kutaka kutoka. Take courage, there is always light at the end of the tunnel
Next Post Previous Post
Bukobawadau