Bukobawadau

MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI MJINI BUKOBA !!

 Ajali iliyohusisha magari mawili imetokea mapema ya leo maeneo ya Rwamishenye (KwaKagambo) mjini Bukoba ,na kusababisha kifo cha mtu mmoja mwendesha pikipiki maarufu kama  (Assecdo) aliyejulikana kwa jina la Kabeya Furgence.
 Mashuhuda wamesema ajali hii imetokea asubuhi ya leo  baada ya Lori aina ya Scania (Semi) yenye nambari T 360 DDU kukatika breki na kuivaa Gari aini ya Fuso yenye nambari T 920 BHW kwa nyuma na kupinduka.
 Inasemekana Dereva wa Semi ilimladhimu kufanya hivyo baada ya kugundua mbele yake kuna Basi la Bunda lililokuwa likitokea stendi kuu ya Bukoba kuelekea Jijini  Mwanza hivyo kufanya maamuzi aliyodhani ni  salama ili kuepuka kugongana na Basi hilo.
Tukio lililopeleka gari hilo aina ya Fuso yenye nambari T 920 BHW ilikuwa imepakia Mchele kupinduka vivyo hivyo na Scania (Semi) yenye nambari T 360 DDU sehemu ya kichwa na nambari za 789 BHW sehemu ya nyuma  nalo kupinduka likiwa limepakiza bidhaa aina mbalimbali.
 Pichani wanaonekana mashuhuda wa ajali hiyo wakiangalia pikipiki iliyopata ajali na kupoteza uhai wa Kabeya Furgence mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya Mkoa Kagera
Mashuhuda wakiangali pikipiki  aliyokua akiendesha Kabeya Furgence aina ya Tvs Star yenye nambari T 270 EGM kabla ya kuanguka na kufunikwa na fuso tukio lililopekea kifo chake akiwa hospitalini.
 Katika ajali hiyo watu wanne wamejeruhiwa na hali zao zinaendelea vizuri
 Muonekano wa  Contena lilikuwa  limebebwa na gari aina Scania (Semi)
 Wananchi wakijunufaisha kwa kuzoa Mchele uliomwagiga baada ya kutokea kwa ajali hiyo mapema ya leo jumatano July 13,2014
 Muonekano wa magunia ya mchele yaliyokuwa kwenye Fuso
 Mashuhuda wakiwa katika hili na lile eneo la tukio
 Mwanamama pishani akiendele kujinufaisha na 'Ekimala Magazi ' mchele uliomwagisha kufuatia ajali hiyo iliyohusisha magari mawili na kupelekea kifo cha mtu mmoja aliyekuwa akienda pikipiki
 Utaratibu wa kufaulisha mzigo ukiendelea
 Haya ndio yaliyojiri katika tukio hili lililotokea asubuhi ya leo July 13,2014
 Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
 Tukio lilimetokea maeneo ya Rwamishenye barabara ya Muleba usawa wa 2.5 Km kabla ya kuingia Bukoba Mjini


Next Post Previous Post
Bukobawadau