Bukobawadau

MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AFANYA ZIARA YA KUSHUTUKIZA KATIKA MRADI WA MAJI KUONA KAMA ALIUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA WATENDAJI

Mhe. Kinawilo wa2AA Pili Akiongozwa na Mhandisi Mtagaywa wa Kwenda Kuhakiki Tenki la Maji Juu.
 Mhe. Kinawilo (wa pili kutoka kulia) aliyeshika Viungio vya Maji Akimhoji  Bw. Dismas Martin Juu ya Ubora wa Viungio vya Mabomba.
 Mhe. Kinawilo Akiwahoji Diwani wa Kata Nyakibimbili Mwenye Baragashia Haji M. Juma na Anayefuata Mwenyekiti wa Kijiji Kitahya Bw J. Kahigwa.JPG
 Tanki Dogo Linalokusanya Maji  Katika Chanzo
 Mhandisi Mshauri Mwesigwa Mtagaywa aliyeinama Akimwonyesha Mhe. Kinawilo Mabomba Yaliyokatwa na Wananchi kama hujuma ya Miundombinu ya Mradi.
Mhe. Deodatus Kinawilo (wa pili kutoka kushoto waliosimama juu ya Tenki) Mara Baada ya Kuhakiki kuwa Pampu Imo ndani ya Tenki
 Tanki Dogo Linalokusanya Maji  Katika Chanzo.


Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawilo afanya ziara ya kushutukiza katika Kata Nyakibimbili Kijijini Kitahya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba leo Agosti 9, 2016 katika chanzo cha maji kilichopo kijijini hapo ili kuhakiki kama pampu ya kusukuma maji  kama ilifungwa na ipo katika tenki la maji lilojengwa katika chanzo hicho cha maji.
Mkuu huyo wa Wilaya aliamua kufanya ziara hiyo ya ghafla na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kuletewa malalamiko na wananchi kuwa siku mradi huo ulipowekewa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw. George Mbijima Julai 27, 2016 maji yaliyotoka katika ghati la Ibwera yalijazwa kwenye tenki na gari la kubebea maji  kwani pampu ya kusukuma maji haikuwepo katika tenki lilipo kwenye chanzo cha maji.
Baada ya kufika katika chanzo hicho cha maji Mhe. Kinawilo aliyeongozana pia na Kaimu  Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Bw. Gregory Fabian,  Mhandisi wa Maji Bw. Dismas Martin, na Mhandisi Mshauri wa Mradi huo Mwesiagwa Mtagaywa wa Kampuni ya (O & A Company Ltd.) alikagua mradi huo na kugundua kuwa pampu ipo na inafanya kazi vizuri ya kusukuma maji.
Aidha, iligundundulika kuwa maji mara baada ya  kusukumwa kutoka kwenye tenki  umbali wa mita 22 kutoka kwenye tenki hilo bomba limekatika kiungio jambo linalosababisha maji kutopanda hadi katika Kata ya Ibwera ambapo Mhe. Kinawilo alimuagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha anamshauri Mkandarasi kufanya marekebisho ya haraka nadani ya wiki moja.
Aidha , katika mradi huo kuliibuliwa suala la wananchi kukata mabomba ya maji katika chanzo hicho na kusababisha maji kutoenda katika tenki linalohudumia vijiji vitatu vya Kitahya, Kibona na Itongo na kusababisha Diwani wa Kata ya Nyakimbimbili Haji Matsawilly Juma kulalamika kuwa maji hayawafikii wananchi na kumwomba Mkuu wa Wilaya kumhimiza Mkandarasi kumaliza kazi ili maji yatoke kwa wananchi kama ilivyotarajiwa.
Maagizo, Mhe. Kinawilo baada ya kushuhudia uharibifu huo alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhakikisha Mkandarasi anafunga vifaa vyenye ubora ili thamani ya vifaa iendane na gharama za mraddi huo. Pili alimwagiza Mwenyekiti wa Kijiji Kitaya   Bw.Johnstone Kahigwa aliyedai kuwa kijiji hakikukishirikishwa tangu mwanzo wa mradi kuhakikisha anashirikiana na Halmashauri ya kijiji chake kuilinda miundombinu ya mradi huo kwa sababu mradi upo katika eneo lake.
Vilevile Mhe. Kinawilo alimwagiza Mhandisi Mshauri kuhikikisha anfanya marekebisho yote ya mradi huo ndani ya wiki moja ili wananchi waanze kupata huduma ya maji. Na mwisho aliwaagiza Watendaji wa Kata za Ibwera na Nyakibimbili kuititsha mkutabno wa pamoja kwa kamati za maji za Vijiji vya Kitaya, Kibona,Itongo na Ibwera ili kuweka mikakati ya kuilinda miundombinu ya mradi huo wa maji.
Mradi huo wa maji ukikamilika unatarajiwa kuhudumia vijiji vinne vya Kitaya, Kibona,Itongo  (Kata Nyakibimbili)na Ibwera (kata Ibwera) una gharama ya zaidi ya shilingi milioni 430 na ulianza katika awamu ya kwanza mwaka 2009 katika upembuzi yakinifu na usanifu, aidha utekelezwaji wake ulianza rasmi  katika awamu ya pili iliyoanza Mwezi Julai, 2013.
Next Post Previous Post
Bukobawadau