Bukobawadau

Anaandika Mzee Ramadhani King

Haya yanayotokea Kagera Je ingekuwa ni mkoa mwingine kama Kusini ama Kaskazi! Je taarifa za habari huwa ni kweli? Leo nimesikia kuwa waathirika wa tetemeko wamekwishagawiwa Mifuko ya saruji na mabati wakati tathmini ikiendelea! Kagera ninayoifahamu mimi kwa miongo saba haijawahi kupatwa njaa! Mara ya mwisho Kagera kupatwa dhoruba hilo ni 1945 hadi 1948 na hiyo ilitokana na vita kuu ya pili ya dunia mimi sijazaliwa bado. Njaa hiyo ilijulikana kwa jina la "ibambura'mabati!
Wakati huu wa tetemeko hili, Kagera hawana njaa bali kinga ya baridi kali usiku na hii mvua nyemelezi! Maneno yanayozagaa ya kubweteka ni kauli zinazoongeza maumivu chuki, sonono na mifadhaiko kutokana na maneno ya kuudhi na kukatisha tamaa. Wana saikolojia watafahamu nini haya hapa juu! Kama ninalala nje na mtu akaja na hema na akasaidia kwa nini nisite kupokea! Uhai wangu ni kipaumbele cha kwanza kuliko siasa!
Wakati huu kwa Bukoba ni baridi sana usiku na mvua kwelikweli! Kagera pia hawasubiri mifuko ya sementi na mabati bali wanalisubiri taifa liuonyeshe mkoa huruma yake kwa moja ya mikoa yake! Aliweza kujenga nyumba bila msaada wa mabati hawezi akabweteka akisubiri misaada! Je unapopewa hema umejengewa nyumba? Tuko nchini mwetu hivyo ni budi huduma ziendelee! Tulikuwa tukifanya kazi kabla ya tetemeko na tunafahamu kwamba maisha yanaendelea na hamna mashaka kama njaa ya 1945-1948 haikuwaua basi tetemeko limepita sukari na chumvi si kipaumbele cha wanakagera bali mahema yawe mengi! Hakika wanaopaswa kushukuriwa zaidi ni TANESCO Kagera kwa jinsi walivyolihimili na kujiweka tayari na tetemeko hili. Mungu awajalie kwani ungelitokea moto basi gharika ingelikuwa ni kubwa mno!

#TetemekoBukoba
Next Post Previous Post
Bukobawadau