Bukobawadau

ATHARI YA TETEMEKO HUKO MISSENYI NI KUBWA


Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dk. Diodorus Kamala ameendelea kutembelea kata moja baada ya nyingine katika kujionea athari ya tetemeke la ardhi jimboni mwake ,ambapo ameweza kushuhidia maeneo mengi na nyumba za watu vilivyoathirika
Tathmini ya haraka inaonyesha jumla ya majeruhi ni 33,Nyumba 167 zimebomoka kabisa,Nyumba424 zimebomoka kuta na jumla ya nyumba 1476 zimepata nyufa na majengo 22 ya taasisi mbalimbali yameathirika.
Wauguzi wa Zahanati ya Ishozi wakitoa huduma nje ya jengo lilipatwa na tetemeko
Hakika ni Changamoto kubwa kama anavyo onekana pichaniMbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala wakati akiendelea kushuhudia namna tetemeko lilivyo athiri majengo ya zahati ya Gera#TetemekoBukoba
Ndani ya Zahanati hiyo hali ndiyo kama hivyo
Muonekano wa Choo cha zahanati ya Ishozi
Camera yetu imeongea na Doktawa Henry Ngaiza wa zahanati ya Ishozi Wilayani Missenyi ili kujua athari na hali ilivyo baada ya tetemeko hilo

Sehemu ya ndani ya Zahati ya Kata ya Ishozi
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa akiendelea kukagua jinzi Jengo la Zahati hiyo lilivyo alibikika vibaya sana
Baadhi ya wanafamilia wakiwa msibani huko Ishozi
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa akitoa heshima zake baada ya akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Bi Pascazia ambaye kifo chake kimetokana na tetemeko hilo lililotokea Sept 10 na kusababisha vifo vya watu 17
Hii ndiyo hali halisi ya wakazi wengi wakiwa wamepoteza matumaini
Diwani wa Kata ya Ishozi, William Rutta akijaribu kutathimini hali ilivyo katika Jengo la Kituo cha Afya Cha Kabyaile Wilayani Missenyi
Akiongea na Bukobawadau Media Mh. William Rutta amesema;'Vyombo vya habari ebu mulika Missenyi ambapo tetemeko la Ardhi lilianzia, Nyumba nyingi sana zimeanguka, Nyumba zimesimama kwa geresha tu ndani ni biscuits, saidieni onyesheni Dunia, leo siku ya sita hata hema moja kwa wahanga hawajaona, mvua zikianza majanga yataongezeka, mazao ya msimu yameshindikana, watz wanalala pasipo na matumaini, takwimu simekuwa kigezo cha kukosa huduma, tuoneeni huruma wananchi wa Kata ya Ishozi wanalalama, wanahabari amieni Missenyi.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji Kigazi kata ya Minziro akibainisha changamoto wanazopambana nazo Wanakijiji cha Kigazi baada tetemeko la ardhi kutokea katika kijiji cha Kigazi. Mojawapo ya changamoto ni ukosefu makazi baada ya nyumba zao kubomoka.

Hapa ni Mutukula ambapo teteeko limeathiri nyumba za wananchi  wengi.


Mwalimu Patrice Israel wa Shule ya Msingi Mutukula katika simanzi kufuatia kubomoka kwa nyumba yake kutokana na tetemeko hilo
Balozi Dr. Kamala akiwafariji wahanga wa tetemeko la Ardhi
Athari ya tetemeko Wilayani Missenyi ni kubwa Zaidi ya kaya 300 hazina makazi,Nyumba 1479 zina nyufa ,majengo ya taasisi 22 yamebomoka ifanyika tathmini ya haraka na kwa uhakika anasema ;Balozi Dr. Kamala .
Ndani ya Nyumba ya Mwalimu Patrice Israel wa Shule ya Msingi Mutukula mara baada ya kupatwa na tetemeko hilo
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa akiendelea kushuhudia kwa macho yake ili aweze kupata cha kuishauri Serikali yake

Maisha yanaendelea katika mazingira magumu

Balozi Dr. Diodorus Buberwa akisaini kitabu cha Wageni alipoitembelea Hospitali ya Mugana.
Mugana Missenyi:pichani ni St.Inviolate Temba akitoa ufafanuzi kwa Mbunge wa jimbo la Nkenge Balozi Dr Kamala atembelea hospital ya Mugana kuwajulia hali majeruhi wa tetemeko la ardhi na kutembelea maeneo mengine Jimboni kujionea athari ilivyo.
Balozi Dr .Kamala ameuambia uongozi wa hospital hiyo kuwa atasaidia kulipa gharama zote za matibabu ya wahanga wa #TetemekoBukoba
Mmoja wa Majeruhi akiwa amelazwa katika hospitali ya Mugana


St.Inviolate Temba anadhibitisha kuwa kifo cha Mtu mmoja Mwanamke Marehemu Bi Anastazia Kahangwa  kilitokea majuzi kati ya Majeruhi 10 waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo
Majeruhi akiwa anaendelea kupata matibabu
Balozi Dr. Kamala akiwajulia hali mmoja wa Majeruhi aliyelazwa katika hospitali ya Mugana
HUKO MISSENYI BALOZI KAMALA ATEMBELEA KIJIJI RUGAZI MINZIRO KUKAGUA MADHARA YA TETEMEKO LA ARDHI
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (aliyevaa miwani) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigazi - akimweleza zaidi ya nyumba 200 zilizoanguka baada ya kutokea tetemeko la ardhi. Pichani ni nyumba ya Mzee John Paulo iliyoanguka baada ya kutokea tetemeko la ardhi. Zaidi ya kaya 300 hazina makazi
Ndani ya Jengo Jipya la Mamlaka ya Mapato (TRA)Mutukula
Taswira nje ya Jengo la (TRA) Mutukula Wilayani Missenyi lililopata tetemeke wakati maafisa wake wakiendelea na kikao na Kamishna mkuu wa TRA hali iliyozua tafrani
Muonekano wa ndani wa Jengo hilo lilipata nyufa
Afisa wa Uhamiaji Mutukula Bwana Shabani akimuonyesha Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala sehemu za jengo hilo lilipata nyufa.
Bwana Shabani katika picha na Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa
Sehemu ya Juu ya Jengo hilo lililopo Mutukula likiwa limepata nyufa maeneo mengi #TetemekoBukoba
Next Post Previous Post
Bukobawadau