Bukobawadau

Mbunge Viti maalum Mama Konchesta Rwamulaza atoa mifuko 70 ya Saruji ili kuwasaidia Waathirika wa Tetemeko

WANANCHI waishio katika mtaa wa Lwome katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameiomba serikali kuwapatia misaada ya hali na mali ili kuwasaidia katika kipidi kigumu walicho nacho.
Hata hivyo kauli hizo zimetolewa na baadhi ya wananchi wakati mbunge wa viti maalumu na Mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema mkoa wa Kagera Mama Konchesta Lwamulaza alipokuwa akitoa pole kwa Ndugu waliopeta jamaa zao wakati wa tetemeko.

Wananchi hao ni pamoja na Jason Rugemalila ambae alimpoteza mama yake wakati wa tetemeko, amesema kuwa toka janga hilo litokee familia hiyo haija wahi kupata msaada wowote.
Pia Anna Kyaruzi amesema kuwa toka tukio hili limetokea katika maeneo yao hakuna msaada wowote ambao wamepewaa kitu ambacho ni chakusikitisha maana misaada inatolewa kwa kuwabagua watu kitu ambao ni hatali kwa jamii.
Naye Mbunge viti Maalum Konchesta Rwamulaza kwa kukushirikiana na wenyeviti wa BAWACHA kutoka katika Wilaya zote za mkoa wa kagera amekabidhi mifuko 70 ya Saruji kwa Mkuu wa wilaya ya bukoba Deodatusi Kinawilo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenelali mstaafu Salimu Kijuu.
Na RENATHA Bukoba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau