Bukobawadau

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aipongeza Serikali ya Mkoa wa Kagera kwa namna ilivyokabiliana na Athari za Tetemeko

#TetemekoBukoba Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa aipongeza Serikali ya mkoa wa Kagera kwa namna ilivyokabiliana na athari za tetemeko
Aahidi mifuko 400 ya cement itakayokabidhiwa kesho kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi,aonyesha kukerwa na mabomu.
 Kauli hiyo ilitolewa na Lowassa wakati alipoingia katika ukumbi wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salimu Kijuu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa siasa pamoja na kiongozi wa dini.
Viongozi hao ni aliekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja, Godbless Lema mbunge wa Arusha mjini,Alhaji Rajabu kutoka katika jumuiya ya kisilamu.

Hata hivyo alisema kuwa Simenti hiyo itakabidhiwa lasimi kesho mapema na Meya wa Manispaa ya Bukoba Chifu Kalumna ili kuendeleza kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi waliopoteza makazi. 
Aidha Lowassa amesema kuwa kuna kila sababu ya serikali kupitia kamati ya maafa kuandaa vipindi maalum kupitia runinga ili kuwafamisha watanzania ukubwa wa tatizo liliopo mkoani Kagera
Pia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Msitaafu Salimu Kijuu ametoa shukrani zake kwa viongozi hao kwa msaada mkubwa wa simenti mifuko 400.
 Katika picha ya pamoja  na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Msitaafu Salimu Kijuu
Credit:Renatha Kipaka,Bukoba.

Next Post Previous Post
Bukobawadau