Bukobawadau

UPEPE MKALI WAEZUA PAA ZA SHULE YA MSINGI BYAMUTEMBA WILAYANI MISSENYI

Shule ya msingi Byamutemba iliyoko kata Nsunga Wilayani Missenyi imefungwa na mkuu wa Wilaya kwa muda wa wiki tatu baada ya vyumba sita vya madarasa kuezuliwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali leo Oct 17,2016 ,Wanafunzi 14 wamejeruhiwa na Wengine wamelazwa Katika Zahanati ya Igayaza
Akidhibitisha kutokea kwa tukio hulo,Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni kanali Denisi Mwilla amesema mvua hiyo ilionyesha a imenyesha leo majira ya saa sita na dakika 25 mchana imeezua Ofisi ya walimu na nyumbamoja ya walimu shuleni hapo ,Makanisa mawili ya Kipentekoste,Jengo la Soko pamoja na nyumba mbili za wananchi
 Jengo la Shule liliezuliwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali.
 Bango la Shule ya Msingi
 Jengo la Darasa lililo ezuliwa na Upepo mkali kufuatia mvua kubwa iliyo nyesha maeneo ya Missenyi hii leo
 Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni kanali Denisi Mwilla akikagua paa za Jengo la Soko lililoezuliwa na Upepo
 Mmoja wa wanafunzi aliyejeruhiwa katika tukio hilo
 Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya msingi Byamutemba iliyoko kata Nsunga Wilayani Missenyi wakiendelea kupata matibabu
 Hili ni Janga jingine!!anakagera TUENDELEE KUMUOMBA MUNGU!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau