Bukobawadau

UN yawapiga msasa wanafunzi wa Chuo cha Tumaini Makumira juu ya SDGs

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akitoa semina juu ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo mkoani Arusha.(Picha na Ferdinand Shayo).

Maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wamefanya ziara ya kutembelea Chuo cha Tumaini tawi la Arusha ikiwa ni pamoja na kutoa semina juu ya Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ikiwemo kufuta umasikini, kuondoa njaa na kuhakikisha upatikanaji wa maji.

Mtaalam wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama amesema kuwa wasomi na wanafunzi walioko vyuoni wanapaswa kuelewa vizuri malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa ili waweze kuyatimiza katika ngazi zao hasa ukizingatia kuwa wanachuo ni wataalamu watarajiwa,na viongozi wa kesho.

Manyama amesema kuwa taasisi,mashirika na jamii pamoja na serikali ina jukumu kubwa la kutekeleza malengo hayo ili kuondoa umasikini, kujenga uchumi endelevu,kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu amesema kuwa vijana hususan wanavyuoni wanapaswa kuwa mambalozi wazuri wa kuyatangaza malengo ya maendeleo endelevu ya UN ili yaweze kutimia na dunia iwe ni sehemu bora zaidi ya kuishi kwa kila mtu.

Temu amesema kuwa UN ina mpango wa kuwafikia vijana walioko vyuoni na mitaani ili waweze kuelewa vizuri juu ya malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na kujua jukumu walilonalo ndani ya malengo hayo.

Na Ferdinand Shayo, Arusha
Mtaalam wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira juu ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) katika ukumbi wa chuo hicho jijini Arusha.Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu (katikati) naRaisi wa Chuo hicho John Maembe (kushoto).
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakifuatilia semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini Arusha.


Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Tumaini Makumira jijini Arusha katika picha ya pamoja na wakufunzi huku wakiwa wameshikilia mabango ya SDGs.
Picha ya pamoja na serikali ya wanafunzi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau