Bukobawadau

UJIO WA HUDUMA YA (SPEED BOAT) KATIKA ZIWA VICTORIA!!

Habari kubwa kutoka katika Chanzo makini ni  Ujio wa Boti mpya inayoenda kwa mwendo kasi (Speed boat) hivi karibuni,kama inavyosemekana kumba huduma ya Boti hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza adha ya Usafiri katika Ziwa Victoria,Boti hiyo ya Kampuni binafsi ya Equetorial Wild Safaris ya nchini Uganda inatalajia kuanza safari zake kati ya Bukoba na Mwanza.Kama inavyo onekana pichani ikiwa katika majaribio ya awali. 
Pamoja na mambo mengi mengine Boti hiyo itakuwa Kichocheo cha kuongezeka kwa watalii wanao pitia Entebe /Uganda  kutembela hifadhi ya Serengeti.

Wakati huo wananchi wa Mkoa wa Kagera wanaendelea kusubilia kwa hamu ahadi ya SERIKALI kuwaletea  meli kubwa  itakayoweza kukidhi haja ya usafiri wa majini iliopo  na tayari Bilioni 21 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya zitakazotumika katika Ziwa Victoria
  #Bukobawadau
Credit photo @tanzanaire
Next Post Previous Post
Bukobawadau