Bukobawadau

CAMERA YETU NDANI YA HOSPITALI YA MKOA

Camera yetu inaangaza Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Mkoa wenye  jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 246, zikiwemo hospitali 13, Vituo vya afya 23na zahanati 210.
Inaonyesha huduma zinaendelea kama kawaida na hali ya mazingira si mbaya kabisa na kwa kupitia tovuti ya Mkoa inaseme;  MKOA wa Kagera kama ilivyo mikoa mingine ya Tanzania unaendelea kutoa ... Huduma kwa Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi .... wazee wanaofika   hasa  katika Hospitali hii ya mkoa
Jitiada zetu za kuonana moja kwa moja na Idara zinayotoa huduma katika hospital yetu
kuanzia Utawala, usimamizi mpaka idara ya ODP kwa wagonjwa wa nje hazikufanikiwa ndipo bukobawadau tukaendelea kufanya kile kinachoweza kuonekana kwa siku ya leo.
 Camera yetu inaangaza kwa kina na kuona hali halisi ndani ya wodi maalumu ya akinamama wajawazito kama inavyoonyesha wengine ulazimika kulala chini.
Hapa swali moja tunaendelea nalo tatizo ni wodi za kulaza wagonjwa hama tatizo ni vitanda...?!
  Tathmini ya haraka haraka inaonyesha katika mkoa wetu wa Kagera asilimia 90 ya hospitali zinazotoa huduma ya TIBA ni za taasisi za dini ikilinganisha na Serikali yenye hospitali moja tu ambayo ni hii ya mkoa iliyopo mjini hapa!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau