Bukobawadau

HEKAHEKA ZA HAPA NA PALE BARABARA YA KASHOZI

 Hii ni barabara ya kashozi  inayokutana na barabara ya kashai ,ni barabara yenye mkusanyiko wa watu wengi ,shughuli nyingi na magari mengi na umaharufu wa barabara hii unazidi kuwepo siku hadi siku ukizingatia ndipo utakapo pita mwili wa Marehemu Cardinal Laurean Rugambwa kutoka parokia ya Kashozi ulipozikwa kwa muda,na kuletwa katika kanisa la jimbo katoliki bukoba, tukio linaloenda kuchukua kasi na kuandika historia mpya katika ukanda huu litakalofanyika tarehe 6/10/2012.Ikiwa ni miaka 15 tangu alipozikwa kwa muda.
Ni barabara moja tegemezi kwa wakazi wa Kashai NHC,kashai halisi ,kilimanjaro,Kisindi,Mafumbo, Kashai Matopeni , Buhembe,kyabitembe, Kahororo, Nyanshenye usawa wa Nyamkazi na vitongoji kadha wakadha...!
Barabara hii nje ya kuwa na shughuli nyingi za kijamii viwanda vya mbao, kiwanda cha samaki cha vic fish,kiwanda cha maji asilia,maghala mbalimbali ya vyakula,Soda na Bia,mashine za kusaga na kukoboa, ,pia inauwelekeo wa shule nyingi  za msingi na sekondari.

Pitapita za hapa na pale barabara ya Kashozi.
 Sehemu ya raia kuvukia (zebra line)nilichokiona hapa bado watu wanatakiwa kuelimishwa juu ya matumizi yake.
Waendesha pikipiki na baiskeri wanachokiangalia wao ni kuwa katika highway.Mistari ya Zebra ni mara chache kuzingatiwa na hili eneo linaongoza kwa ajali za mara kwa mara kama sio kila siku.
Next Post Previous Post
Bukobawadau