Bukobawadau

MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE APATIKANA NI EUGENE FABIAN

Miss Eugene Fabian (katikati)kutokea mkoa wa Mara ndiye mshindi wa shindano la Redd,s Miss Lake Zone 2012,Lililofanyika usiku wa jana  mjini kahama na kuwashirikisha warembo kutoka mikoa 6 ya kanda ya ziwa.

  Redd's Miss Lake Zone 2012, Miss Eugene Fabian katika picha ya pamoja na mshindi wa pili na watatu katika shindano hilo ambalo warembo wa mkoa wa Kagera hawakuweza kutamba kabisa,ambapo nafasi ya tatu imechukuliwa na Miss Happiness Rweyemamu kutoka  mkoa wa Shinyanga (pichani kushoto)na mshindi wa pili ni Miss Happiness Daniel(kulia) kutoka Mwanza. Washindi hawa watatu watawakilisha Kanda ya ziwa katika shindano la taifa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao. Zawadi kwa mshindi wa kwanza ni  kitita cha shilingi Laki 7, mshindi wa pili laki 5 na mshindi wa tatu laki nne na nusu !!!

Washiriki katika  atua ya kumi bora kuumi bora
Msimamo wa tano bora. 
Mshindi wa Redd's Miss Lake Zone akivalishwa Taji
 
Mzee Hashim Lundenga (a.k.a Uncle Hashim) akitoa angalizo katika mashindano haya.

Miss Kagera 2012 Miss Baby Kalalaa akiwakilisha vyema katika shindano la Redd's Miss Lake Zone kwa kucheza na nyoka na kuweza kushinda kama Miss Talent.
Kwa wale wakazi wa bukoba bila shaka bado mnakumbuka  ilivyokuwa katika shindano la Miss Kagera kufuatia uwezo mkubwa alioonyesha  Miss Baby Kalalaa  katika kucheza ngoma za asili,pichana anawakilisha  kivingine zaidi.
Mdau Jamal Kalumuna mmoja wa kamati ya Miss Lake Zote akitoa salaam
Next Post Previous Post
Bukobawadau