Bukobawadau

KUWASILI KWA MWILI WA BALOZI JOSEPH RWEGASIRA MJINI BUKOBA MARCH 7,2016

Ndugu Julius (Tibaijuka) Rwengasira pichani ambaye ni mmoja wa watoto wa Marehemu Mzee Joseph Rwegasira akiwa amebeba Msalaba mara baada ya kuwasili kwa mwili wa mzee wetu, mpendwa wetu  Balozi Joseph Clemence Rwegasira katika Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba
 Ndege maalum zilizobeba wanafamilia na Mwili wa Marehemu Mzee Rwegasira
 Mjane wa Marehemu Mzee Rwegasira katika hali ya simanzi
 Marehemu Balozi Joseph Rwegasira (81) ni Waziri zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kifo chake kimetokea juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mwili wake ukaagwa Jana katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter, Oysterbay Jijini Dar  na kuwasili leo Jumatatu March 7,2015 Mjini Bukoba kwa ajili ya Shughuli ya mazishi itakayofanyika kijijini Kanyigo Bukoba
 Baadhi ya waombolezaji waliofika Uwanjani kwa ajili ya mapokezi
 Jeneza lenye Mwili wa Balozi Joseph Rwegasira likitolewa kwenye Ndege maalum ya Shirika la Auric Air
 Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Balozi Joseph Rwegasira ukiingizwa kwenye Gari Maalum

Vilio vikitawala kwa Wanafamilia
 Wanafamilia wakiwa kwenye majonzi makubwa ya kuondokewa na Mpendwa wao
 Ni Simanzi kubwa kwa wanafamilia na waombolezaji mara baada ya mwili kuwasili.
 Mzee Kalvin na Mzee Deo wakiwa wamefika Uwanjani ushiriki mapokezi ya mwili wa Balozi Joseph Rwegasira 
 Nje ya Uwanja wa Ndege vilio na vikitawala ,pichani kulia ni Bi Joanitha,biinti wa marehemu
 Bwana Rahym Kabyemela akimfariji Mjane wa Marehemu pichani (kulia)
 Kushoto ni Bwana Optaty Henry
Selfie kutoka Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba
 Mara baada ya Mwili kuwasili Nyumbani kwa Marehemu Kijijini Kanyigo
 Poleni sana wafiwa, tulimpenda mzee wetu lakini, Mungu amempenda zaidi
 Kama inavyo onekana katika picha ni vilio, majonzi na simanzi vikitawalazaidi kwa waliohudhuria Nyumbani Jioni hii na wanafamilia kwa ujumla.
 Ni Simanzi na Vilio nyumbani kwa marehemu Kijijini Kanyigo
 Mwonekano wa picha wa Marehemu Mzee Rwegasira aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara, na baadaye waziri wa Kazi na mwisho Waziri wa mambo ya nchi za nje,na Mbunge wa Nkenge mpaka mwaka 2000
 Muonekano wa Jeneza lenye Mwili waMzee  Joseph Rwegasira
 Muendeleze wa matukio yaliyojiri Mjini Bukoba mpaka Kijijini Kanyigo
Nyuso za mazonji na Vilio mwanzo mwisho... 
 BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043,0715 505043 ,0768 397241
 .........Endelea kuwa nasi kwa matukio zaidi ya  picha......................

Next Post Previous Post
Bukobawadau